Jamhuri yakata rufaa kupinga Tido Mhando kuachiwa huru
Upande
wa Jamhuri katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha
serikali hasara ya Sh.milioni 887.1, umekata rufaa Mahakama Kuu kupinga
uamuzi wa kuachiwa huru Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.
Mahakama
hiyo ilimwachia huru Mhando na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye
alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia
haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hata
hivyo, Wakili wa Serikali Leonard Swai alidai kuwa Jamhuri haujaridhika
na hukumu hiyo kwamba pamoja na kwamba mikataba inadaiwa kuwa
haikufuata sheria lakini mawakili walilipwa fedha,hasara ambayo
imesababishwa na na mshtakiwa.
Rufaa hiyo inasubiri kupangiwa jaji na tarehe ya kusikilizwa.
Katika
kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia
madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni
887.1.